St.
Catherine of Siena Catholic Church,
Kitisuru
Sunday 29th January 2023
Announcements
1. Today is the Fourth Sunday in
Ordinary Time. We take this opportunity
to thank the following groups for their
service today:-
●8.00a.m.
Mass: St. Elizabeth
●10.00a.m.
Mass: Choir/St. Michael
●12.00 noon
Mass: St. Teresa
2. Next Sunday will be the Fifth Sunday
in Ordinary Time. CWA will be on duty in
all the three Masses.
3. We shall have a special Second
Collection Next Sunday, February 5th
2023 to support our Brothers and Sisters
in our Outstation, St. Martin de Porres
- Kibagare in
their fundraising drive for Choir
equipment. Kindly consider to support
them.
4. CWA will begin formation classes for
the new members on Sunday, February 19th
2023. Ladies who would like to join CWA
are encouraged to register at the parish
office after Mass or in the course of
the week, Tuesday to Saturday.
5. Catechism classes for both children
and adults are conducted as follows:
a) Children: Every Saturday at 2PM and
Sundays after the 10.00a.m. Mass.
b) Adults: Every Saturday at 3PM.
6. Pilgrimage to the Holy Sites: Both
the Parish Priest and Eclairer
Pilgrimage Agency, wish to let you know
that there still few chances for those
who would wish to participate in this
year's
scheduled spiritual pilgrimages to Holy
Land on 4th to 16th March, and Europe on
9th to 20th May respectively. Those
interested are welcome to register with
us.
7. Young Christian Adults (YCA) would
like to invite all persons within the
age bracket of 25-45 years to join their
group. They meet briefly every Sunday
after the 10.00a.m. Mass under the
avocado tree near the church notice
board.
8. Lady of Hope Wellness Institute
wishes to thank all Parishioners and
people of God in our Parish for the
incredible support received towards the
preparation of their 9th annual walk.
The walk took place successfully
yesterday. Thank you one, thank all!
9. All Ecclesial groups will meet next
Sunday after the 10.00a.m. Mass. All
interested members are encouraged to
join these various groups.
10. Saints of the Week:
Date Feast/Solemnity
Tuesday, 31st January 2023 St. John
Bosco, priest, memorial
Thursday, 2nd February 2023 The
Presentation of the Lord, Feast
Friday, 3rd February 2023 St. Blaise
St. Ansgar
11. We take this opportunity to welcome
any new person visiting our Parish for
the first time. (Request them to either
stand up or raise their hands and invite
the parishioners to welcome them with a
warm clap)
Find these announcements on our website
and on our notice board.
THANK YOU FOR WORSHIPPING WITH US AND
FOR YOUR SUPPORT TO OUR CHURCH. HAVE A
BLESSED WEEK
Kanisa Katoliki La Mt.
katerina wa Siena, Kitisuru
Matangazo ya Jumapili, Januari
29, 2023.
1. Leo ni Jumapili ya nne ya kipindi cha
kawaida cha kanisa. Tunatoa shukrani za
dhati kwa makundi yafuatayo yaliyohudumu
katika ibada zetu:-
●Misa ya Saa 2
Asubuhi: Jumuia ya Mt. Elizabeti
●Misa ya Saa 4
Asubuhi: Kwaya na Kundi la Sala la Mt.
Mikaeli
●Misa ya Saa 6
Adhuhuri: Jumuia ya Mt. Teresa
Jumapili ijayo itakuwa ya tano ya
kipindi cha kawaida cha kanisa. Chama
cha Wanawake Wakatoliki, CWA, kitahudumu
katika misa zote tatu.
2. Jumapili ijayo, Februari 5, tutafanya
mchango maalum kwa kutoa sadaka ya pili,
kuwasaidia ndugu zetu wa parokia ndogo
ya Mt. Martin de Porres-Kibagare,
kununua ala za muziki na vifaa vingine
vya Kwaya. Tafadhali jiandaee kuwapa
mchango wako.
3. Chama cha Wanawake Wakatoliki, CWA
kitaanza mafunzo ya wanachama wapya,
jumapili ya Februari 19 mwaka huu.
Kinadada ambao wangependa kujiunga na
CWA, wanaweza kusajiliwa katika ofisi ya
parokia baada ya misa, au saa za ofisi
kati ya Jumanne na Jumamosi.
4. Mafunzo ya dini yaani Katekasia ya
Watoto na Watu wazima yanaendeshwa
ifuatavyo:
c) Watoto: Kila Jumamosi saa 8 alasiri,
na Jumapili baada ya misa ya saa 4
asubuhi.
d) Watu Wazima: Kila Jumamosi saa 9
alasiri.
5. Hija kwenda Maeneo Matakatifu: Baba
Paroko na Shirika la Eclairer Pilgrimage
Agency, wanakufahamisha kwamba kuna
nafasi chache zimesalia za kushiriki
safari ya kwenda kuhiji Nchi Takatifu
kati ya Machi 4 na 16, na Bara Uropa Mei
9 hadi 20 mtawalia. Wanaotaka kushiriki
wanaombwa kujisajili ofisini.
6. Chama cha Vijana Wazima, Young
Catholic Adults (YCA), kinawaalika
wakristo wote wa umri wa miaka 25 hadi
45 kujiunga na chama hiki.
Young Adults hukutana kwa dakika chache
kila Jumapili, baada ya misa ya saa 4
asubuhi, chini ya mparachichi yaani
avocado tree, karibu na ubao wa
matangazo.
7. Taasisi ya Lady Hope Wellness, inatoa
shukrani za dhati kwa Wakristo wote na
watu wengine wa matabaka tofauti, kwa
kuwapiga jeki katika maandalizi ya
Makala ya 9 ya matembezi ya kukabili
Saratani. Matembezi yalifana sana jana.
Asanteni sana!
8. Makundi yote ya Elkesia kanisani
yatakutana Jumapili ijayo, baada ya misa
ya saa nne asubuhi. Waumini wote
wanahimizwa kujiunga na makundi
yanayowafaa na wanayopenda.
9. Watakatifu wa Wiki:
Tarehe Maadhimisho/Sherehe
Jumanne, Januari 31, 2023 Ukumbusho wa
Mt. John Bosco, padre.
Alhamisi, Februari 2, 2023 Sherehe ya
Kupokelewa kwa Kristo.
Ijumaa, Februari 3, 2023 watakatifu
Blaise na Ansgar
10. Na sasa ni fursa ya kumkaribisha
muumini yeyote anayeshiriki katika ibada
ya hapa kwetu kwa mara ya kwanza. (Muombe
kusimama au kuinua mkono alipo, na
wakristo wamkaribishe kwa makofi )
Unaweza kupata matangazo haya katika
tovuti yetu na ubao wa matangazo.
ASANTE KWA KUABUDU NASI NA KULISAIDIA
KANISA LETU. TWAKUTAKIA WIKI YENYE
BARAKA TELE
Get in Touch With Us